Ijumaa, 4 Agosti 2017

Sh 30,000/- zamfikisha kortini


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mara imemfi kisha katika Mahakama ya Wilaya ya Bunda, (jina linahifadhiwa) kwa makosa ya kudai na kupokea rushwa ya Sh 30,000.
Mwalimu huyo wa Shule ya Msingi Nyambitilwa iliyoko Kijiji cha Misisi, Kata ya Sazira wilayani Bunda, aliomba na kupokea rushwa ya Sh 30,000 kwa mzazi (jina linahifadhiwa) wa mtoto anayesoma darasa la pili hapo (jina linahifadhiwa) ili asichukue hatua za kisheria dhidi ya mzazi huyo kwa kosa la utoro wa mwanawe.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mara, Holle Makungu, awali wakati wa likizo ya Juni mwaka huu, mtoto huyo wa darasa la pili na baba yake walikwenda mkoani Kagera kusalimia ndugu na jamaa, lakini hawakurejea mapema hadi shule zikafunguliwa kutokana na kuugua kwa mtoto huyo wakiwa mkoani humo.
Baada ya mtoto huyo kupata nafuu, walirejea Bunda na mtoto akaenda shule kwa nia ya kuendelea na masomo yake na alipofika shuleni alirejeshwa nyumbani na kutakiwa kuja na mzazi wake.
Baba wa mtoto huyo iliitika mwito na alipoonana na Mwalimu huyo na alitakiwa atoe rushwa ya Sh 30,000 ili mtoto huyo aendelee na masomo la sivyo angechukuliwa hatua za kisheria. Mzazi huyo hakuwa na fedha hizo, hivyo akaona atoe taarifa Takukuru ambao mtego wa hongo hiyo uliandaliwa na kumnasa mtuhumiwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni