Mwanamume mmoja
mweusi ambaye anadaiwa kulazimishwa kuingia ndani ya jeneza na wanaume
wawili wazungu ambao walitishia kumchoma akiwa hai ametoa ushahidi mbele
ya mahakama nchini Afrika Kusini.
Victor Mlotshwa aliangua kilio kwenye mahakama kuu ya Middleburg wakati alikumbuka kisa hicho cha mwezi Agosti mwaka uliopita.Mahakama ilicheza video ya kisa hicho ambapo bwana Mlotshwa anaweza kusikika akilia na kuomba washambuliaji kumsamehe.
Anadai kuwa wakulima Theo Jackson na Willem Oosthuizen walimfunga kwa nyaya wakampiga na kutishia kumpiga risasi.
Wanasema kuwa lengo lao lilikuwa ni kumshikisha adabu. Kisa hicho kilizua ghadhabu kubwa nchini Afrika Kusini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni