Mhubiri mtata Gilbert Deya amerudishwa nchini Kenya ambapo anakabiliwa na makosa ya usafirishaji wa binadamu.
Bwana Deya aliwasili nchini Kenya siku ya Ijumaa akiwa kwenye ndege ya Kenya Airways.Kurudishwa kwake ni baada ya rufaa yake ya kupinga kurudishwa nchini Kenya kukataliwa na mahakama ya Uingereza.
Muhubiri huyo ambaye anamiliki kanisa moja eneo la Peckham kusini mashariki mwa mji wa London.
Amekuwa katika orodha ya watu wanaosakwa kwa usafirishajzi wa binadamu tangu 2004.
Mwaka 2014, mahakama moja ya London ilimwachilia mhubiri huyo kwa mashtaka ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono. Amekana mashtaka yote.
Mkewe bi Mary Deya alifungwa jela mwaka 2014 baada ya kupatikana katika kitengo cha watoto katika hospitali ya Kenyatta 2005.
Alihukumiwa kifungo cha miaka 3 na jaji wa mahakama kuu Msagha Mbogholi.
Kaimu Jaji Grace Nzioka alikuwa amemfunga Mary 2011 kwa wizi wa mtoto mmoja na kutoa habari za uwongo lakini alikata rufaa dhidi ya shtaka hilo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni