Jumapili, 17 Agosti 2014

VICTOR MOSES AHAMA CHELSEA KWENDA STOKE CITY

Big move: Victor Moses poses with his new No 13 shirt at the Britannia Stadium after completing his move

Victor Moses akipozi katika picha na jezi namba 13 atakayotumia katika uwanja wa Britannia baada ya kukamilisha usajili wake.

WINGA wa Chelsea,Victor Moses amejiunga na Stoke City kwa mkopo wakati huu Jose Mourinho anasuka kikosi chake kuelekea msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England ulioanza kutimua vumbi leo.
Moses alitazamiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Mreno huyo kutokana na kiwango alichoonesha katika fainali za kombe la dunia akiwa na Nigeria nchini Brazil, majira ya kiangazi mwaka huu, lakini badala yake atacheza chini ya kocha Mark Hughes katika dimba la Britannia .
Mnigeria huyo msimu uliopita alikuwa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Liverpool, lakini alikosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Brendan Rodgers kilichokuwa kikisaka ubingwa na kuzidiwa kete na Manchester City

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni