Simu ya Samsung yaingiza maji
Simu ya kisasa ya
Samsung Galaxy S7 inayopigiwa upatu kuwa na uwezo wa kustahimili kuwa
chini ya maji imefeli majaribio ya shirika la moja la kutathmini ubora
wa bidhaa za kielektroniki.
Programu ya simu hiyo ya Samsung Active ilizima punde baada ya kutumbukizwa ndani ya pipa la maji.Kampuni hiyo ya kutathmini ubora wa bidhaa, Consumer Reports ilirudia jaribio hilo kwa mara ya pili wakitumia simu tofauti na kama ile ya kwanza ikafeli.
Kampuni ya kutengeneza simu hiyo ya Samsung ikijitetea imesema huenda simu hizo zilikuwa ni mbovu na hivyo kuruhusu maji kuingia ndani.
Hati hiyo maalum inathibitisha kuwa simu hizo zinauwezo wa kustahimili kutumbukizwa ndani ya maji.
Consumer Reports iligonga vichwa vya habari kote duniani ilipotambua kuwa simu aina ya Iphone 4 ilikuwa na matatizo ya ya kifaa cha kuungia mbali.
''kwa kawaida tumekuwa tukiamini pale mtengezaji wa bidhaa akituambia kuwa bidhaa yake inaweza kustahimili hata kutumbukizwa ndani ya maji, lakini leo tulipojaribu kuhakiki madai ya Samsung tuligundua kuwa simu hizo zinazima baada ya kutumbukizwa ndani ya pipa la maji ''
''Bila shaka wale walionunua simu hizo kwa imani kuwa haitoharibika hata baada ya kutumbukizwa ndani ya maji, watalazimika kutafuta ridhaa kutoka kwa watengenezaji,,,''
Mwaka uliopita Sony, iliwaonya watumiaji wa bidhaa zake kuwa kulikuwa na uwezekano kuwa simu zake zitaharibika zikitumika ndani ya maji.
Samsung inatarajiwa kutangaza faida kubwa zaidi baada ya mauzo yaliyozidi matarajio ya simu hiyo aina ya Galaxy S7.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni