Jumatatu, 11 Julai 2016

MJUE EDER ALIYEWAPA WARENO KOMBE LA EURO 2016

     Eder
    Kabla ya fainali ya michuano ya Euro 2016 kati ya Ufaransa na Ureno kuanza, wengi walikuwa wakimzungumzia mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.
    Lakini hali ilibadilika baada ya Ronaldo kuumia na kulazimika kuondoka uwanjani, huku akitokwa na machozi.
    Kwa wengi, kitumbua cha Ureno kilikuwa kimeingia mchanga. Lakini, baadaye kulijitokeza shujaa mwingine. Huyu si mwingine ila ni Eder ambaye amjina yake ni Éderzito António Macedo Lopes

      Eder
    Eder nusura aumie muda mfupi baada ya kuingia uwanjani
    Mashabiki wengi wa soka duniani, walimfahamu mshambuliaji mtata, Eder, aliyefunga bao la ushindi dakika ya 109 na kuzamisha ndoto ya Wafaransa uwanja wa Stade de France, Paris.
    Eder aliingia nafasi ya kiungo wa kati Renato Sanches.
    Haya hapa ni mambo muhimu kumhusu Eder.
    1. Jina lake kamili ni Éderzito António Macedo Lopes, Macedo likiwa jina la ukoo wa mamake na Lopes jina la ukoo wa babake.
    2. Eder alizaliwa tarehe 22 Decemba 1987 mjini Bissau nchini Guinea-Bissau, taifa lililotawaliwa na Wareno hadi lilipojinyakulia uhuru 1974.
    3. Ana umri wa miaka 28 na anasema Ronaldo alimwambia angefunga bao. “Alinipa moyo na nguvu, na hilo lilikuwa muhimu.”
    4. Kimo cha Eder ni futi 6 na inchi 3.
    5. Alihamia Ureno akiwa mtoto soka yake ya kulipwa alianza kucheza mara ya kwanza klabu ya Academica 2008 kabla ya kujiunga na klabu ya Braga miaka minne baadaye ambapo aliwika sana.
    6. Alichezea klabu ya Swansea mwaka 2015 baada ya kununuliwa £5 milioni kutoka Braga. Mechi yake ya kwanza Ligi ya Premia ilikuwa sare ya 2-2 dhidi ya mabingwa watetezi wa wakati huo Chelsea alipoingia nafasi ya Bafetimbi Gomis. Hakufunga bao lolote Swansea na akatumwa klabu ya Lille ya Ufaransa inayocheza Ligue 1 kwa mkopo kipindi kilichosalia cha msimu.
      Eder
      Ronaldo akimpongeza Ederbbada ya mechi hiyo
  1. Eder alijiunga rasmi na Lille kwa mkataba wa kudumu Mei mwaka huu baada ya kuwasaidia kufuzu kwa Europa League.
  2. Katika uchezaji wake Ligi Kuu ya Ureno, alicheza jumla ya mechi 143 na kufunga mabao 38.
  3. Eder amechezea timu ya taifa ya Ureno tangu 2012 na aliwachezea Kombe la Dunia 2014.
  4. Alifungia Ureno bao lake la kwanza la kimataifa mechi yake ya 18, mechi ya kirafiki dhidi ya Italia katika uwanja wa Stade de Geneve Juni 2015.          chanzo: BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni