Uchina inatafuta mamba 100 waliotoroka kutoka kwenye hifadhi moja baada ya mafuriko makubwa
Mamlaka nchini
Uchina inajaribu kutafuta takriban mamba 100 waliotoroka kutoka kwenye
hifadhi moja baada ya mafuriko makubwa yanayoshuhudiwa nchini humo.
Mafuriko hayo yaliwawezesha mamba hao kuogelea na kuondoka kwenye eneo lilizingirwa kwenye hifadhi hiyo katika mkoa wa Anhui.Hata hivyo mamba huwindwa kutokana na ngozi yao inayouzwa kwa bei ghali mno pamoja na nyama yao na pia hutumika kuwaburudisha watalii.
Zaidi ya watu milioni moja wamelazimika kutorokea maeneo yenye milima ilikutoroka mafuriko yanayochacha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni