Jumapili, 17 Agosti 2014

ARSENAL YAANZA VEMA LIGI YA UINGEREZA

Dakika za lala salama: Aaron Ramsey wa Arsenal akiifungia timu yake bao la ushindi.
WASHIKA bunduki wa London, Asernal chini ya kocha mkuu, Mfaransa, Aserne Wenger wameanza ligi kuu England kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika uwanja wa Emirates.
Palace walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 35’ kipindi cha kwanza kupitia kwa Brede Hangeland, lakini katika ya 45’,Laurent Koscielny aliisawazishia Asernal bao hilo.
Katika dakika ya 90’, Aaron Ramsey aliifungia Asernal bao la pili na la ushindi.
Kikosi cha Arsenal: Szczesny, Debuchy, Chambers, Koscielny, Gibbs (Monreal 53), Wilshere (Oxlade-Chamberlain 69), Arteta, Sanchez, Ramsey, Cazorla, Sanogo (Giroud 62).
Wachezaji wa akiba: Rosicky, Martinez, Campbell, Coquelin.
Kadi ya njano: Chambers, Cazorla.
Kikosi cha Crystal Palace: Speroni, Kelly, Dann (Delaney 75), Hangeland, Ward, Puncheon, Jedinak, Ledley, Bolasie (O'Keefe 90), Chamakh, Campbell (Gayle 85).
Wachezaji wa akiba: McCarthy, Hennessey, Murray, Bannan.
Kadi ya njano: Puncheon, Chamakh, Kelly.
Kadi nyekundu: Puncheon.

Mwamuzi: Jon Moss (W Yorkshire)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni