Kundi la wapiganaji wa kiisilamu nchini Nigeria Boko Haram, wameuteka mji mwingine Kaskazini Mashariki ya nchi hiyo.
Mji huo Michika ulio katika jimbo la Adamawa, ulitekwa siku ya Jumapili , siku mbili baada ya mji jirani wa Gulak kutekwa pia na wapiganaji hao.
Wakazi wa Michika waliotoroka vita walisema walipigwa na mshtuko na kulazimika kutoroka kwani wapiganaji walikuwa wanapiga risasi watu kuholela walipowasili katika magari yao.
Walioshuhudia mapigano hayo walisema kuwa wapiganaji hao walijificha ndani ya nyumba za wakazi waliokuwa wametoroka vita pale ndege ya kijeshi ilipokuwa inazunguka eneo hilo kuwatafuta wapiganaji hao.
Jeshi la Nigeria limesema kuwa lilifanikiwa kuwaua wapiganaji 50 wa Boko Haram, katika makabiliano makali katika jimbo la Borno (TK).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni