Waziri wa
Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (kushoto) akiangalia meno ya tembo katika
Kituo cha Kikosi cha Kupambana na Ujangili (KDU) cha Kanda ya Kati, kilichopo
Wilaya ya Manyoni mkoani Singida. Meno hayo yalikamatwa mkoani Singida na
Dodoma. Picha na Salim Shao.
KIKOSI cha Kupambana na Ujangili Kanda ya Kati (KDU)
kimefanikiwa kukamata vipande 59 vya meno ya tembo vikiwa na uzito wa zaidi ya
kilo 200 vyenye thamani ya Sh176.7 milioni sawa na tembo 29. Katika msako huo watu saba
walikamatwa baada ya kukutwa na meno hayo, akiwamo ofisa mtendaji wa Kijiji cha
Kayui wilayani Manyoni, Philomen Kanyonga aliyedaiwa kuongoza ujangili huo.
Akielezea tukio hilo kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro
Nyalandu juzi, mhifadhi mwandamizi wa Ngorongoro, Robert Mande alisema meno hayo
yalikamatwa Machi 28 na 31.
Alisema kikosi kazi hicho kilianza
kufuatilia mtandao wa ujangili katika kijiji cha Kiyombo na walifanikiwa
kukamata meno hayo 53 ya tembo 26 katika kijiji hicho pamoja na bunduki aina ya
SMG yenye namba 40129 ambayo alikamatwa nayo Eliud Selemani.
Alisema
katika tukio hilo waliwakamata watuhumiwa watano ambao aliwataja kuwa ni Idd
Waziri (29), Leonard Oscar (32), Ramadhani Said (40) na mtendaji huyo ambao wote
walikutwa na meno hayo 53 ya tembo.
Mhifadhi huyo alisema katika
kijiji cha Chinangali mkoani Dodoma walifanikiwa kukamata watuhumiwa wawili
ambao ni David Makasi na Joseph Malima ambao walikutwa na meno sita yenye uzito
wa kilo 31.1 yakiwa na thamani ya sh 27.3 milioni baada ya kuuawa kwa tembo
watatu.
Baada ya kupokea maelezo hayo, Waziri Nyalandu alisema
anataka kuona watuhumiwa hao wanahojiwa ili kujua watu wanaowatuma kufanya
ujangili huo kwa kuwa sasa anataka kukamata majangili wakubwa ambao wamekuwa na
mtandao mkubwa wa kuteketeza tembo nchini.
Alisema katika
kuhakikisha wanaboresha ufanisi wa idara ya wanyamapori, wako katika mchakato wa
kuifanya idara hiyo kuwa mamlaka inayojitegemea, ili kuweza kupambana na
majangili hao.
“Hawa majangili wananiumiza kichwa kila siku; wanaua
tembo wetu kwa ubinafisi wao,” alisema.
Sasa nataka nikamate
majangili wakubwa kabisa wanaoendesha mtandao huu wa kumaliza tembo na pia sasa
tuko katika hatua ya mwisho kwa ajili ya kuifanya idara ya wanyamapori kuwa (TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni