Jumapili, 10 Agosti 2014

TISHIO LA EBOLA: WANANCHI WAANDAMANA NCHINI LIBERIA


Maafisa wa polisi wavunja maandamano nchini Liberia


Polisi wa kukabiliana na ghasia nchini Liberia wamevunja maandamano dhidi ya vile serikali inavyolichukulia swala la kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola.

Waandamanaji waliokasirika waliweka vizuizi katika barabara kuu na kusema kuwa serikali haichukui miili ya waathiriwa wa ugonjwa huo.

Shirika la Afya Duniani WHO limeutaja ugonjwa huo kama wa dharura na hatari katika kipindi cha miongo minne.

Guinea imefunga mpaka wake na Sierra Leone na Liberia, huku Nigeria ikitoa wito kwa watu waliojitolea kusaidia kusitisha ueneaji wa ugonjwa huo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni