WATU wanane wamekufa papo hapo, wengine tisa
wakijeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Nyangao mkoani Lindi baada ya gari
aina ya Land Rover, mali ya Halmashauri ya Mji Masasi kupata ajali katika kijiji
cha Mtama wilaya ya Lindi Vijijini mkoani hapa.
Gari hilo lenye namba za
usajili STL 1615, lilikuwa linatokea Lindi ambako maofisa wa Halmashauri ya
Masasi walikuwa wanashiriki katika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yaliyofanyika
kitaifa katika Viwanja vya Ngongo, nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.
Kutokea kwa ajali hiyo
kulithibitishwa jana na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga
aliyesema ilitokea juzi majira ya saa 11.30 jioni katika kijiji cha Mtama.
Aliwataja waliokufa kuwa ni Issa
Salumu (33), Malik Selemani (24), Juma Ausi (21), Rajab Khalfan (17), Said
Mchora (24) na Fadhili Mchalasi (26) ambapo watu wawili hadi sasa hawajafahamika
majina yao, na amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi.
Marehemu wote ni wakazi wa kijiji cha Mtama. Kwa mujibu
wa Kamanda Mzinga, waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo ni dereva wa gari hilo, Kessy
Mwaijande (40).
Pia wamo madiwani
watano wa Halmashauri ya Mji Masasi ambao ni Habiba Amlima, Maimuna Chiputa,
Exaveria Mhagama, Asha Abbas na Blandina Nakajumo.
Wengine ni Abraham Mohammed, Shaabani Issa Kitemwe na
Ally Adam, wote wakazi wa kijiji cha Mtama.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga.
Mbuzi wakiwa wamezagaa ovyo katikati
ya barabara eneo la sabasaba Manispaa ya Morogoro na kuleta kero kwa watumiaji
wa barabara hiyo.PICHA NA MAKTABA/ MTANDA BLOG.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mashuhuda
wa ajali hiyo walisema kuwa majira ya jioni kwenye eneo hilo la tukio, waliliona
gari hilo likiwa kwenye mwendo kasi, mazingira ambayo yalisababisha dereva wa
gari hilo aliyekuwa akijaribu kukwepa mbuzi waliokuwa barabarani kushindwa
kumiliki gari hilo na hatimaye kuacha njia na kuwagonga watu waliokuwa pembezoni
mwa barabara hiyo, waliokuwa wakifanya biashara ndogo.
Hata hivyo, mmoja
wa mashuhuda hao, Ahmad Mbonde aliiambia HabariLeo Jumapili kuwa, kama si
kuwakwepa mbuzi, dereva wa gari hilo asingesababisha ajali.
Kutokana na
tukio hilo, Kamanda Mzinga amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama
barabarani ili kunusuru maisha ya watu wanaoendelea kupoteza maisha na huku
wengine wakibaki na ulemavu, mazingira ambayo hupunguza nguvu kazi ya
Taifa.HABARILEO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni