Jumanne, 7 Januari 2014

EUSEBIO AZIKWA KWA HESHIMA ZOTE URENO

 

GOODBYE EUSEBIO. A hearse carrying the coffin of late Portuguese soccer legend Eusebio da Silva Ferreira drives slowly during funeral ceremonies at Luz stadium in Lisbon, Portugal, 06 January 2014. Tiago Petinga/EPAKWAHERI EUSEBIO. Gari iliyobeba mwili wa Gwiji la Soka Eusebio da Silve Ferreira likipita polepole katika uwanja wa Luz  mjini Lisbon, Ureno , tarehe 6 January 2014.
Makumi ya maelfu ya waombolezaji walijitokeza kwenye mazishi ya Gwiji la mpira wa mihuu Eusebio licha ya mvua kali kunyesha.ambaye alizaliwa Msumbiji na hatimaye kuwa mchezaji mahiri wa soka duniani.
Waombolezaji walijipanga kando kando ya barabara za mji wa Lisbon na wakawa wanashangilia wakati gari iliyobeba mwili wake iliyofungwa kwa vtambaa vyekundu na vyeupe ambazo ni rangi za klabu yake ya zamani Benfica,na kutangazwa moja kwa moja na Luninga ya nchi hiyo.

Kabla ya hapo mashabiki wapatao10,000 walishangilia kwa nguvu wakati jeneza la Eusebio lilipowekwa katikati ya uwanja tadium of Light ambao ni wa Klabu ya Benfica muda wa dakika chache kabla ya kuzungushwa uwanjani kwa gari wakati wimbo wa  Andrea Bocelli "Con te partiro" kutoka Italia  ukiimbwa

Waombolezaji wengi wao wakilia machozi walirusha skafu za rangi nyekundu na nyeupe ambazo ni za klabu ya Benfica ambayo Eusebio aliichezea enzi za uhai wake na wengine kupeperusha bendera ya taifa ya wakiimba : "Eusebio, Eusebio".
"Eusebio alikuwa katika dunia hii kama kina Cristiano Ronaldo na Lionel Messi. Ataendelea kuwa mioyoni mwa mashabiki wa Benficas milele," alisema kocha wa  Benfica Jorge Jesus.

Bendera zilipepea nusu mlingoti kufautia serikali ya Ureno kutangaza siku 3 za maombolezo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni