Jumatatu, 11 Agosti 2014

SABABU YA MBUNGE WA CHADEMA KURUDI BUNGENI HIZI HAPA

Arfi
Na Magreth Kinabo, Dodoma
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Said Arfi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)amezitaja sababu za kurejea katika bunge hilo, kuwa ni hofu ya Mwenyezi Mungu.
Aidha Arfi ameitaja sababu nyingine ni kwamba amerudi katikaBunge hilo, ili kuhakikisha kwamba anaisadia nchi kupita katika mchakato wa Katiba mpya kwa amani na utulivu kwa kutumia kipaji chake na kuwatumikia Watanzania.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na mjumbe huyo, wakati akihojiwa na kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Shirika la Utangazaji la Tanzania(TBC).
Akizungumza katika kipindi hicho, huku akinukuu kitabu cha Nabii Musa, Arfi alisema Mwenyezi Mungu hapendezwi na mtu mwenye jeuri na anayejivuna.
“Nimejitathimini na kuona mimi mwenyewe ni nina nafasi gani… maaskofu, mapadre, wachungaji na masheikh. Viongozi wetu wametusii turudi turudi napata kiburi wapi cha kutokurudi,” alihoji Arfi.
Akirejea katika kitabu cha Qruan anasema Mwenyezi Mungu hapendezwi na mtu mwenye kiburi na anayejivuna.


Aliongeza kuwa viongozi hao “ wana nafasi kubwa pia wanaheshima ndio maana nimeweza kurudi,””alisema.
Mjumbe huyo alisema sasa ni wakati wa kila mtu kueleza ukweli, kwani amerejea katika Bunge hilo, amepata bahati ya kuchangia katika sura ya nne katika kifungu cha 43na 44 kinachohusu haki za msingi.
“Nimepata fursa ya kutoa mapendekezo ya haki za wazee nisingewezakuwasilisha kama ningekuwa nje. Pia haki za wafanyakazi,” alisema.
Akizungumzia kuhusu wajumbe wenzake waliosusia Bunge hilo, aliwataka kutanguliza maslahi ya taifa.Huku akisisitiza kwamba atajitahidi kuwashawishi wajumbe walioko nje ya Bunge hilo ili waweze kurejea.
Arfi aliwahakikishia wananchi kuwa wanawatengenezea Katiba itakayowasaidia kubadilisha ya watu wote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni