.jpg)
Nipende kuwashukuRu vijana wenzangu na hasa kwa wale wanaopenda kusoma makala zangu.Tuzidi kuombeana uhai. leo napenda kuongelea kuhusu swala la kujishugulisha ambalo wengi limekuwa likiwasumbua sana hasa kwa sisi vijana. Nimekutana na vijana wengi ambao wamemaliza Masomo yao wakiwa na matumaini ya kupata kazi kubwa na kukaa maofisini lakini kwa bahati mbaya wakawa bado hawajapata kazi na kuhisi labda wana tatizo. Ukweli ni kawaida kwa mambo kama hayo kutokea kwa sababu kwa sasa hivi kila mtu anatafuta kazi na wengi hupenda kazi zenye mishahara
Mikubwa. Tunaishi katika kipindi ambacho mashindano na ubinafsi umekua wa kasi sana kwa sababu wengi huwapa kazi ndugu jamaa na marafiki hata kama hawana vigezo vya kutosha.
Ndio maana utaenda ofisi nyingine ukakuta ni kubwa na zenye muonekano mzuri lakini hawana huduma
Bora zenye kuridhisha. hivyo huku ukisubiri kuna vitu ambavyo unaweza ukajituma ili uweze kujiingizia
Kipato hata kama kitakuwa kidogo lakini ni bora kuwa na hicho kuliko kukosa kabisa.
Hivyo napenda kuwashauri vijana wenzangu ambao mmemaliza masomo na wamekuwa wakitafuta kazi kwa
muda mrefu kwamba unaweza ukajishugulisha na kitu chochote chema na chenye maendeleo huku
ukisubiria bahati yako ya kupata kazi.
Usivunjike moyo kwa sababu hujapata kazi na kila wakati unapopata
Wazo la kukata tamaa mshukuru Mungu kwa kuwa kuna wale ambao hawakupata uwezo wa kwenda hata
Darasani. Tukutane tena katika makala yetu ijayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni