Mwanamume aliyewalaghai watu kwa kuwauzia mvinyo bandia, Rudy
Kurniawan, 37, amefungwa jela kwa miaka kumi na kuamrishwa kulipa faini ya dola
milioni 20 kwa kosa hilo.
Rudy aliuza Mvinyo ghushi wenye thamani ya mamilioni ya dola bila ya
kujulikana kwa miaka mingi.Bwana Kurniawan ni mtu wa kwanza kuwahi kwenda jela kwa kuuza mvinyo bandia nchini Marekani.
Alipatikana na hatia ya kuchanganya mvinyo wa zamani na mvinyo wa mpya nyumbani kwake. Baada ya kuinchanganya aliuza Mvinyo huo kwa bei ghali mno akidai kuwa ni Mvinyo wa kipekee.
Vibandiko bandia alivyotumia bwana Kurniawan kuwahadaa waekezaji kununua bidhaa zake vilipatikana nyumbani kwake.
Kashfa hii aliifanya tangu mwaka 2004 hadi 2012 kulingana na viongozi wa mashitaka.
Mwezi Disemba alipatikana na hatia ya kuwalaghai watu kwa nja ya posta.
Kama raia wa Indonesia, Bwana Kurniawan atarejeshwa nchini Indonesia ili akafunguliwe mashitaka huko. Tayari amekuwa jela kwa miaka 2 tangu kukamatwa mwaka 2012.
Mnamo mwaka 2006, inaaminika kwamba aliuza chupa 12,000 za mvinyo bandia katika mnada.
Lakini maafisa wakuu walisema kuwa walipata maelfu ya vibandiko vya mvinyo mzuri zaidi wa Burgundy na Bordeaux pamoja na chupa ambazo hazikuwa zimwekwa vifuniko nyumbani kwake
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni