Mtu mmoja kusini
mwa Msumbiji katika mkoa wa Inhambane alilazimika kumlipia mahari mkewe
aliyefariki wikendi iliopita kulingana na chombo cha habari cha taifa.
Baada
ya mkewe kufariki kutokana na matatizo ya kujifungua, nduguze
walimlazimisha mpenziwe kulipa ''Lobolo'', wakionya kwamba la sivyo
hatozikwa.Nduguze walimshutumu kijana huyo kwa kushindwa kuafikia majukumu yake ikiwemo kutambulishwa kwa jamaa na ndugu za mwanamke huyo kabla ya janga hilo kutokea.
Ili kuhakikisha kuwa mazishi hayo yanafanyika, kijana huyo alilazimika kumnunulia nguo na viatu marehemu mkewe, kukubali kulipa zaidi ya dola 800 (sawa na shilingi za Kitanzania1,760,000) na kufanya haruasi mnamo tarehe 15 mwezi Disemba.
Nduguye kijana huyo Irmao do Jovem alielezea matatizo yao.
''Tulijaribu kuchangisha fedha walizotaka, lakini tuliweza kuchangisha dola 178 (sawa na shilingi za Kitanzania 387,200) tu. Hivyobasi ilibidi kuweka ahadi ya kulipa fedha zilizosalia siku ya harusi''.
Huku ikiwa familia ya kijana huyo imekubali kulipa, walishutumu tabia ya familia ya mwanamke huyo.
Hatahivyo, ni utamaduni miongoni mwa makabila mengi nchini Msumbiji hususan iwapo mwanamume anaamua kuishi na mwanamke bila kufuatilia utamaduni wa kumuoa mwanamke huyo.
Hili ni funzo kwa vijana wengi ambao wanapenda kuishi na wanawake bila kujitambulisha kwa wazazi wa mwanamke husika na kufunga nao ndoa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni