AJALI TENA MORO : LORI LAACHA NJIA NA KUTUMBUKIA MTARONI
Lori la mafuta aina ya Scania lenye namba za usajiri T772 BAZ
limetumbukiakwenye mtaro eneo la Kihonda barabara kuu ya Morogoro Dodoma
baada ya dereva wa Lori hilo kushuka na kuliacha gari hilo bila kulizima na
kuwafukuza wezi waliokuwa juu ya tenk la gari hilo wakishusha mizigo. Dereva wa Lori hili alipofika pele kwenye tuta alishuhudia pikipiki
ikiwasha taa na kuzima aliamua kuongeza umakini na kubani kwamba mmoja wa
abiri aliyekuwa kwenye pikipiki hiyo alipanda juu ya Tenk na kushusha
maboksi ya Oil ndipo dereva huyo aliposhuka akajisahau kuvuta
'handbreak' hivyo wakati anapambana nao lori liliendelea kutembea na kuingia kwenye mtaro. Dereva huyo anasema kuwa wezi hao walifanikiwa kukimbia na boksi moja la oil.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni