Ijumaa, 13 Desemba 2013

PINDA,NIPO TAYARI KUNG’OLEWA NIKIBAINIKA NI MZIGO

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amevunja ukimya na kusema yuko tayari kuachia ngazi endapo tu Rais Jakaya Kikwete ataamua kumwondoa na kama itatokea hivyo, atamshukuru Rais kwa kumwambia, ahsante. Mhe Pinda aliliambia Bunge mjini Dodoma jana kwamba endapo Rais hatafanya hivyo, bado wabunge wanayo mamlaka ya kikatiba ya kumwondoa kwa njia ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye kulingana na Ibara ya 53 A(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu endapo itaungwa mkono na waheshimiwa wabunge  
habari kutoka bungeni kupitia blog ya MATUKIO NA MICHAPO 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni