Wabunge nchini
Uganda wamepigana ndani ya ukumbi wa bunge wakiwa katika siku ya pili
ya kikao cha kujadili wa muswada wa kuondoa ukomo wa miaka ya kugombea
nafasi ya urais kwa mjibu wa katiba ya taifa hilo.
Katika ugomvi
huo wabunge hao walirushiana viti, kuharibu vipaza sauti katika kikao
hicho kilichoongozwa na Spika wa bunge, Bi.Rebecca Kadaga.

Wabunge hawa wanadai kuwa kama kikomo cha umri wa miaka 75 kitaondolewa basi rais aliyepo kwa sasa atapata mwanya wa kugombea tena mwaka 2021.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni