Ukivalia viatu vyako bila soksi unajiweka katika hatari ya kupata matatizo makubwa zaidi kuliko kunuka miguu pekee.
Chuo
cha Tiba ya miguu nchini Uingereza kinasema karibuni kumekuwa na
ongezeko la maambukizi ya maradhi yanayosababishwa na kuvu (fangas) kutokana na
kuvuma kwa mtindo wa kuvalia viatu bila soksi, hasa miongoni mwa vijana.Mtaalamu Emma Stephenson anasema amekuwa akipokea wanaume wa kati ya miaka 18-25 walio na matatizo kwenye miguu yao ambayo yametokana na kutovalia soksi au kuvalia viatu visivyowatosha vyema.
Kutovalia soksi siku hivi kumekuwa mtindo maarufu wa mavazi, na mwanamuziki Sam Smith ni miongoni mwa watu wanaojitokeza hadharani wakiwa na viatu bila soksi.
Wanaume wengi katika maonesho ya mitindo pia mara nyingi huonesha mavazi wakiwa na viatu bila soksi.
Mwanamuziki Tinie Tempah amejishindia tuzo nyingi kwa sababu ya mitindo na mara nyingi katika maonesho ya mitindo ya London huketi viti vya mbele.
Yeye pia huwa mara nyingi havai soksi - lakini anafahamu madhara yake?
"Unyevu mwingi na joto unaweza kusababisha maambukizi ya maradhi yanayotokana na kuvu mfano ugonjwa unaosababisha muwasho na kuchubuka kwa ngozi (kwa Kiingereza athlete's foot)."
Kwa mujibu wa Emma, madhara yake yanaweza kuwa mabaya.
"Moja ya vitu vibaya nilivyowahi kukumbana navyo ni cha mwanamume mmoja wa miaka 19 aliyefanya kazi ya kuosha magari. Miguu yake ilikuwa inatokwa na jasho sana na ilikuwa imechubuka sana."
Lakini bila shaka itachukua ujasiri kumwambia bingwa wa UFC Conor McGregor kwamba anaweza kupata matatizo kutokana na mtindo wake wa kuvalia viatu.
Emma anashauri kwamba siri ni kutozidisha, iwapo bado utataka kutovalia soksi.
Jaribu usivae viatu bila soksi kwa muda mrefu.
Jaribu pia kuweka kitu cha kukausha jasho kwenye soli ya kiatu chako kabla ya kukivalia bila soksi.
Kadhalika, kuwa makini kuchunguza miguu yako. Ukigundua unaumwa pahali mwone daktarii upesi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni