Ajali hiyo ya moto imeripotiwa kutokea majira ya jioni (Jumatatu) katika gereza la Nyakiriba, katika wilaya ya Rubavu mpakani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Uokozi haukutosha
Akiongea na BBC kwa njia ya simu mkuu wa wilaya hiyo, Sheikh Hassan Bahame, amesema kuwa juhudi za uokozi zimefanyika haraka ila mahabusu 3 walifariki na wengine 44 kupatwa na majeraha ya moto.Majeruhi walifikishwa mara moja katika hospitali kuu ya wilaya.
Amesema kuwa kutokana mazingira ya milima ambapo gereza hilo limejengwa, imekuwa vigumu kwa wazima moto kufanya kazi yao kwa wepesi na haraka.
Shekh Bhame ameelezea hasara iliyojitokeza.'' Hasara kubwa ambayo imetokea ni vifo vya hawa wafungwa. Na majeraha waliyopata wafungwa wengine. Kuna vitu vingi vimeharibika na hatujajua idadi yake bado.''
Sheikh Bahame ametahadharisha kuelekeza lawama la shambulio la kigaidi akisema kuwa japo inatia shaka, ni muhimu uchunguzi zaidi kufanywa.
''Hata sisi tunajiuliza, mbona mambo haya yametokea, na juzi tu yametokea Muhanga?Inatakiwa uchunguzi wa ndani zaidi ufanywe. Lakini uhakika bado hatujapata.'' Amesema Sheikh Bahame.
Uchunguzi umeanzishwa kujua chanzo cha moto, pamoja na ule moto katika gereza la Muhanga mwezi mmoja uliopita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni