Ramadhani Singano 'Messi' akishangilia baada ya kuifungia bao la ushindi Simba SC |
Simba SC
sasa inafikisha pointi 44 baada ya kucheza mechi 25, wakati Azam inabaki
na pointi zake 45 za mechi 24 katika nafasi ya pili. Tayari Yanga SC
imekwishajihakikishia ubingwa baada ya kufikisha pointi 55 za mechi 24
Simba SC
sasa itaanza kuiombea dua mbaya Azam FC ipoteze mechi zake zote mbili
zilizobaki dhidi ya Yanga na Mgambo- na wenyewe (Simba SC) washinde
mechi yao ya mwisho, ili kumaliza katika nafasi ya pili waweze kucheza
Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.Katika mchezo huo, uliochezeshwa na
refa Israel
Nkongo
wa Dar es Salaam aliyesaidiwa na Frerdinand Chacha wa Mwanza na Soud
Lila wa Dar pia, mabao ya Simba SC yalifungwa na Ibrahim Hajibu na
Ramadhani Singano ‘Messi’, wakati la Azam FC lilifungwa na Mudathir
Yahya.
Dalili za
Azam FC kupoteza mchezo huo zilianza kuonekana mapema tu baada ya
dakika ya 38, kiungo wake tegemeo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kutolewa
kwa kadi nyekundu kufuatia kumchezea rafu Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.
Na
mwishoni mwa kipindi cha kwanza, Frank Domayo akaumia na kushindwa
kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Brison Raphael.
Emmanuel Okwi kulia akimtoka Serge Wawa wa Azam FC leo |
Simba SC ilipata bao lake la kwanza dakika ya 48, mfungaji Hajibu aliyemalizia kwa kichwa krosi ya kiungo Said Ndemla.
Mudathir
Yahya akaisawazishia Azam FC dakika ya 57 akimalizia pasi ya Kipre
Herman Tchetche na dakika ya 74, Messi wa Msimbazi akaifungia Simba SC
bao la pili kwa shuti la mbali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni