Jumanne, 7 Januari 2014

MAN U YATOLEWA KOMBE NJE LA FA, YAPIGWA 2-1 NA SWANSEA

article-2534083-1A6FC0C100000578-313 634x3931 c4cf8

MIKOSI imeendelea kumwandama kocha mpya wa Man U David Moyes, baada ya timu yake ya Manchester United kufungwa mabao 2- 1 na Swansea katika Raundi ya tatu ya Kombe la FA na kutolewa. (HM)

 

Bao lililoizamisha United iliyocheza pungufu ya mchezaji mmoja lilifungwa na Wilfried Bony dakika ya mwisho na Mashetani Wekundu wa wanatolewa katika raundi ya tatu kwa mara pili ndani ya miaka 30.

 

Javier Hernandez aliisawazishia United dakika ya 17 baada ya Wayne Routledge kuifungia Swansea bao la kuongoza dakika ya 12.

 

Katika mchezo mwingine, Liverpool imeifunga mabao 2-0 Oldham na kusonga mbele mabao ya Iago Aspas dakika ya 54 na Tarkowski aliyejifunga dakika ya 84.

Chanzo: binzubeiry

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni