Mshambuliaji
wa kimataifa wa uingereza Daniel Sturridge amesema upasuaji wa nyonga
uliofanyika leo kule nchini Marekani umefanikiwa na anatarajia kupona
haraka na kurudi katika majukumu yake ya klabu ya Liverpool.Mshambuliaji
huyo alikutana na jopo la madaktari bingwa nchini marekani baada ya
kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara msimu huu na kumfanya akose
michezo mingi sana ya timu yake ya Liverpool na timu ya taifa.
Mchezaji
huyo wa zamani wa Chelsea alipost katika ukurasa wake wa instagram
kwamba ”nahitaji kuwajulisha wote kwamba upasuaji umeenda vizuri na
napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kuliwezesha hili” Aliandika katika
ukurasa huo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni