Mwigizaji
maarufu wa filamu za Bollywood nchini India Salman Khan amekuhumiwa
kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtu
mmoja asiye na makazi alipokuwa akiendesha gari huku akiwa amelewa
mjini Mumbai.
Khan alikuwa ameshtakiwa kwa kuua bila kukusudia
baada ya kuelekeza gari lake kwenye kundi la watu waliokuwa wamelala
kwenye njia kando ya barabara mwaka 2002. Mmoja kati ya watu hao Noor
Ullah Khan alikufa katika ajali hiyo.Khan amedai kuwa dereva wake ndiye anayepaswa kulaumiwa lakini mashuhuda wanasema mwigizaji huo ndiye aliyekuwa kwenye usukani na alikimbia baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Kwa mujibu wa jaji wa mahakama hiyo mwigizaji huyo anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni