Mfuasi wa Chadema akiwa chini baada ya ‘kukatwa mtama’
na mfuasi mwingine wa chama hicho baada ya kutokea vurugu baina ya wafuasi
wanaounga mkono uongozi na wale wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe jana
baada ya kuahirishwa kwa hukumu ya kesi ya mbunge huyo katika Mahakama Kuu,
Kanda ya Dar es Salaam jana. Picha na Silvan Kiwale
DAR ES
SALAAM.
WAFUASI wa Chadema wanaomuunga mkono aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe na wanaounga mkono uongozi wa juu, jana walitwangana tena muda mfupi baada ya kuondoka eneo la Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
WAFUASI wa Chadema wanaomuunga mkono aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe na wanaounga mkono uongozi wa juu, jana walitwangana tena muda mfupi baada ya kuondoka eneo la Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Tukio hilo limetokea huku Mahakama hiyo
ikiahirisha hadi leo, kutoa uamuzi wa maombi ya Zitto kuzuia kujadiliwa na
Kamati Kuu ya Chadema.
Katika maombi hayo namba 1 ya mwaka 2014,
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, anaiomba Mahakama iizuie Kamati
Kuu ya Chadema kumjadili na au kuchukua uamuzi wowote kuhusu uanachama wake hadi
kesi yake ya msingi aliyoifungua mahakamani hapo itakaposikilizwa na kutolewa
uamuzi.
Uamuzi wa maombi hayo ulipangwa kutolewa
jana na Jaji John Utamwa ambaye hata hivyo, alisema alikuwa hajamaliza kuandika
uamuzi huo na kuahirisha shauri hilo hadi leo mchana.
Maombi hayo ya Zitto ya zuio la muda la
kujadiliwa na kuchukuliwa uamuzi wowote kuhusu uanachama wake yametokana na kesi
ya msingi aliyoifungua mahakamani hapo Januari 2, 2014, dhidi ya Bodi ya
Wadhamini wa Chadema na Katibu Mkuu wa chama hicho.
Katika kesi hiyo, Zitto pia anaiomba
Mahakama Kuu imwamuru Katibu Mkuu wa Chadema ampatie mwenendo na taarifa za
kikao cha Kamati Kuu za kumvua nyadhifa zake zote alizokuwa nazo ndani ya chama
na iwazuie walalamikiwa kumwingilia katika utekelezaji wa majukumu yake ya
ubunge wa Kigoma Kaskazini.
Mapigano
Baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo,
wanachama wa makundi yote waliondoka eneo la Mahakama wakiendelea kuimba na
kushangilia lakini walipofika eneo la Mahakama ya Rufani ghafla walianza
kupigana ngumi na mawe. Baadhi yao walikamatwa na askari kutokana na vurugu
hizo.
Awali, wafuasi hao walifika mapema asubuhi
katika viwanja vya Mahakama tayari kusikiliza uamuzi
huo.
Ulinzi ulikuwa umeimarishwa na askari polisi
wakiwamo wale wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), waliokuwa na silaha pamoja na
mabomu ya machozi walikuwa wametanda.
Pia kulikuwa na askari wa Kikosi cha Mbwa
pamoja na gari la maji ya kuwasha.
Licha ya kuwahi, ni wafuasi wachache
walioruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi wa Mahakama tena baada ya kuandikisha
majina yao huku wakitambuliwa na viongozi wao waliokuwapo. MWANANCHI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni