DAR
ES SALAAM.
MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono ametoa ufafanuzi juu ya uhusiano wake na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.
MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono ametoa ufafanuzi juu ya uhusiano wake na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.
Hatua hiyo ya Mkono imekuja baada ya
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu kumtuhumu kuwa aliwahi kumpa Zitto
magari mawili.
Katika taarifa yake aliyoitoa jana, Mkono
alisema kuna magari mawili yanayohusishwa na Zitto na kuyataja kuwa ni Toyota
Land Cruiser na Nissan Patrol.
“Sijawahi kumpatia Zitto magari, isipokuwa
kuhusu hiyo Land Cruiser, nilitoa msaada wa kuwanusuru Zitto na Mbowe
(Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe), kule Tarime kwenye msiba wa marehemu
Chacha Wangwe (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Chadema), kwani walikuwa wakitishiwa
kupigwa.”
Alisema alitoa gari hilo lililokuwa na
Bendera ya Bunge liwachukue Mbowe na Zitto na kuwapeleka Mwanza... “Walipofika
Mwanza, Zitto aliwasiliana na mimi kuhusu ununuzi wa gari hilo na kupitia wakala
wangu nilimuuzia,” alisema Mkono.
Kuhusu Nissan Patrol, Mkono alisema
lilikodishwa kwa Zitto na mpaka sasa bado analipa gharama za
kulikodisha...
“Hata nyaraka za umiliki wa gari hili ninazo
mimi mwenyewe kama mmiliki halali. Ninamiliki magari mengi tu hata wewe
mwandishi ukitaka Vogue (aina ya gari) nitakukodisha tu,” alisema
Mkono.
Alisema wanafahamiana kwa siku nyingi hata
kabla ya Zitto kuwa mbunge na kwamba aliwahi kufanya mazoezi kwa vitendo katika
ofisi yake (Mkono), alipokuwa mwanafunzi.
Kuhusu tuhuma kwamba anawahonga wapinzani
wake wajitoe katika uchaguzi ili apite bila kupingwa alisema katika Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2000, 2005 na 2010 alipita bila kupingwa kutokana na uchapakazi
wake wa kiwango kikubwa.
Mkono pia alijibu tuhuma zilizotolewa na
Zitto jana kwamba Mbowe alipewa mamilioni ya fedha na Mkono kwa nyakati tofauti
na kusema hajawahi kutoa fedha zozote kusaidia
Chadema.
Zitto akana
Katika hatua nyingine, Zitto ameitaka
Chadema kumwandikia mashtaka mapya yaliyoibuliwa na Lissu ili aweze kujitetea.
MWANANCHI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni