Alhamisi, 2 Februari 2017

DAWA YA KUKABWA USINGIZINI USIKU HII HAPA

Image result for Photo of a sleeping person
Mtu aliyelala na kuhangaika huku akikabwa

Kuota ndoto mbaya ni jambo la kuchokesha sana. Hili ni tatizo linalowapata watu wengi sana. Mtu anapoota ndoto mbaya anaweza kuamka akiwa na hofu kubwa, kuchanganyikiwa, kukata tamaa na maisha,  hasira kubwa na woga mkubwa na kadhalika.

Ndoto hizi zinaweza kuwa na matukio ya kukosa amani hatari na hata kuhamanika (panic). Waathirika wa ndogo hizi mbaya wanapozinduka wanakuwa katika hali ya kuchanganyikiwa na inawachukua muda kupata usingizi tena.
Ndoto hi mbaya zinaweza kusababishwa na mambo yafuatayo:
  • kulala vibaya kama kujikunja sana, kupindisha shingo kwa kutumia mto mkubwa sana
  • kuwa na homa inayoanza
  • kuwa na msongo wa mawazo
  • kuwa na mhemko (anxiety)
  • kutumia baadhi ya madawa makali kabla tu ya kulala.
  • kula vyakula vigumu kabla ya kulala mfano ugali mgumu
  • Sababu za kibinadamu (wanga)
Nini kifanyike?
Mambo ya kufanya kuepuka hali hii ni haya yafuatayo:
  • Uwe na utaratibu wa kulala ukiwa umejinyoosha bila kujikunja sana
  • kuangalia kama una homa
  • kujitahidi usiwe na msongo wa mawazo 
  • kukwepo mihemko
  • kujitahidi kukwepa kutumia madawa makali na kwenda kulala saa hiyo hiyo
  • kukwepa kula vyakula vigumu kabla ya kulala iwapo ni mlaji wa ugali jitahidi uwe mlaini au kuwepo na muda mrefu baada ya kula kabla ya kulala. 
  • Iwapo hizo zote hazisaidii basi inawezekana ni tatizo la kibinadamu (wanga) hivyo cha kufanya ni kugeuka ulivyolala kama kichwa kilikuwa magharibi geuka kichwa kielekee mashariki na kadhalika. 
NINI MAONI YAKO ? 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni