Mwanamke mmoja wa
miaka 23 kutoka nchini Afghanistan ameielezea BBC kwamba mumewe
alimfunga kamba na kumkata masikio yote mawili katika mzozo wa
kiunyumba katika mkoa wa kaskazini wa Balkh.
Mwanamke huyo Zarina kwa sasa yuko hospitalini akipata matibabu na hali yake inaendelea nzuri''Sijatenda dhambi lolote'' ,alisema.''sijui kwa nini mume wangu alinifanyia hivi''.
Mume huyo kwa sasa ameenda mafichoni katika Ulaya kufuatia shambulio hilo kulingana na maofisa wa polisi.
Zarina ameambia chombo cha habari cha Pajhwok kwamba shambulio hilo ambalo anasema halikusababishwa na hatia yoyote lilifanyika baada ya mumewe kuamka.
Mwanamke huyo aliolewa akiwa na umri wa miaka 13 na ameiambia BBC kwamba uhusiano wake na mumewe haukuwa mzuri.
Zarina alilalamika kwamba mumewe alijaribu kumzuia kuwatembelea wazazi wake na amesema hataki kuwa naye tena.
"Ananishuku sana na kila mara hunituhumu kwa kuzungumza na wanaume wengine wakati ninapoenda kutembelea wazazi wangu'' ,alisema.
Zarina anataka akamatwe na kushtakiwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni