Jumatano, 22 Aprili 2015

Watu 10 Wafariki Dunia Baada ya Basi la kampuni ya Unique Kugongana na lori la Coca Cola

Habari zilizotufikia zinaarifu kuwa basi la Unique lenye namba za usajili T148 BKK likitokea jijini Mwanza kwenda Tabora limegongana uso kwa uso na lori la kampuni la Cocacola katika kijiji cha Ibingo kata ya Samuye Shinyanga.
Watu 10 wamefariki na 50 wamejeruhiwa.Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni