Rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi amehukumiwa kifungo cha miaka 20
jela kwa makosa ya kusababisha kuuliwa waandamanaji mwaka 2012.
Korti ya makosa ya jinai mjini Cairo imetoa hukmu hiyo wakati Morsi na
watuhumiwa wengine katika kesi hiyo-wengi wao wakiwa viongozi wa chama
cha Udugu wa kiislam-wakisimama ndani ya tundu la vigae ndani ya ukumbi
wa mahakama katika chuo cha mafunzo ya polisi mjini Cairo.
Kesi yao inahusu matumizi ya nguvu yaliyotokea nje ya kasri la rais mwezi Desemba mwaka 2012. Wafuasi wa Morsi waliwashambulia waandamanaji wa upande wa upinzani na kusababisha machafuko yaliyopelekea watu wasiopungua 10 kuuawa.
Jaji Ahmed Youssouf ameachilia mbali madai ya kuchochea mauaji ya waandamanaji wawili na mwandishi habari mmoja machafuko hayo yalipolipuka mbele ya kasri la rais-madai ambayo wadadisi wengi walikuwa wakifikiriaa yangepeleka Morsi kuhukumiwa adhabu ya kifo.
Morsi na watuhumiwa wenzake wakumbusha yaliyotokea katika msikiti wa Rabaah al Adawiya
Akitoa hukumu hiyo jaji Ahmed Youssouf ameyataja majina ya mtuhumiwa wote na kufafanua: "Mohammed Mohamed Mursi, Mohammed el Baltagy na Essam el Erian wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa ushiriki wao wa kuchochea mauwaji ya umma wa wamisri na tuhuma za kulidhuru taifa la Misri."
Morsi na watuhumiwa wenzake walinyoosha vidole vinne-alama inayokumbusha malalamiko yaliyofanywa katika msikiti wa Rabaah al Adawiya ambako polisi waliingia kwa nguvu wakawaua mamia ya waandamanaji wafuasi wa Morsi Agosti 14 mwaka 2013.
Kesi zilizosalia dhidi ya Mursi hazitaharakishwa
Morsi anakabiliwa na kesi nyingine nne pamoja na wanachama wenzake wa udugu wa kiislamu, tangu alipopinduliwa na wanajeshi Desemba mwaka 2013. Morsi na wenzake wana nafasi ya kukata rufaa dhidi ya hukumu ya leo.
Wadadisi wanahisi viongozi wa Misri hawatofanya pupa kusikiliza kesi nyengine kwa kuwa hakuna ghasia majiani na wafuasi wa Udugu wa kiislamu hawakusanyiki kwa wingi ili kuepusha wasikamatwe.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/AP/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
Kesi yao inahusu matumizi ya nguvu yaliyotokea nje ya kasri la rais mwezi Desemba mwaka 2012. Wafuasi wa Morsi waliwashambulia waandamanaji wa upande wa upinzani na kusababisha machafuko yaliyopelekea watu wasiopungua 10 kuuawa.
Jaji Ahmed Youssouf ameachilia mbali madai ya kuchochea mauaji ya waandamanaji wawili na mwandishi habari mmoja machafuko hayo yalipolipuka mbele ya kasri la rais-madai ambayo wadadisi wengi walikuwa wakifikiriaa yangepeleka Morsi kuhukumiwa adhabu ya kifo.
Morsi na watuhumiwa wenzake wakumbusha yaliyotokea katika msikiti wa Rabaah al Adawiya
Kiongozi wa Udugu wa kiislam, Mohamed Badie, aliyehukumiwa adhabu ya
akifo, anapelekwa mahakamani akasikilize hukumu ya wanachama wenzake wa
udugu wa kiislam.
Mbali na Mohamed Morsi, wakuu wengine 12 wa chama cha Udugu wa
kiislamu na wafuasi wa itikadi kali akiwemo Mohammed el Beltagy na Essam
el Erian, nao pia kila mmoja amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.Akitoa hukumu hiyo jaji Ahmed Youssouf ameyataja majina ya mtuhumiwa wote na kufafanua: "Mohammed Mohamed Mursi, Mohammed el Baltagy na Essam el Erian wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa ushiriki wao wa kuchochea mauwaji ya umma wa wamisri na tuhuma za kulidhuru taifa la Misri."
Morsi na watuhumiwa wenzake walinyoosha vidole vinne-alama inayokumbusha malalamiko yaliyofanywa katika msikiti wa Rabaah al Adawiya ambako polisi waliingia kwa nguvu wakawaua mamia ya waandamanaji wafuasi wa Morsi Agosti 14 mwaka 2013.
Kesi zilizosalia dhidi ya Mursi hazitaharakishwa
Morsi anakabiliwa na kesi nyingine nne pamoja na wanachama wenzake wa udugu wa kiislamu, tangu alipopinduliwa na wanajeshi Desemba mwaka 2013. Morsi na wenzake wana nafasi ya kukata rufaa dhidi ya hukumu ya leo.
Wadadisi wanahisi viongozi wa Misri hawatofanya pupa kusikiliza kesi nyengine kwa kuwa hakuna ghasia majiani na wafuasi wa Udugu wa kiislamu hawakusanyiki kwa wingi ili kuepusha wasikamatwe.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/AP/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni