Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini amewaomba raia wa kigeni kubakia nchini
humo wakati wakati akikatisha ziara yake ya kiserikali nchini Indonesia
kushughulikia wimbi hilo la chuki dhidi ya wageni.
Wiki tatu za ghasia zinazoongezeka dhidi ya wageni nchini Afrika kusini
zimesababisha kiasi watu sita kuuwawa na kuwalazimisha wahamiaji 5,000
kutafuta hifadhi katika makambi ya muda.
Machafuko hayo , ambayo yameanzia katika mji wa mashariki wa bandari wa Durban kabla ya kusambaa katika maeneo mengine ya nchi hiyo, yanabeba ghasia za hisia za chuki dhidi ya wageni ambazo ziliikumba Afrika kusini mwaka 2008 wakati watu 62 walipouawa.
Katika tukio la hivi karibuni kabisa, polisi siku ya Jumamosi (18.04.2015) wamesema wageni waliouwawa wamefariki kutokana na kuchomwa visu mjini Alexandra, mji ulioko kaskazini mwa Johannesburg. Eneo hilo linaloishi watu masikini limekuwa lengo ya ghasia nyingi katika siku hiyo, ambapo maafisa wa polisi walifyatua risasi za mipira kuwatawanya watu waliokuwa wakifanya uporaji.
Zaidi ya watu 30 wamekamatwa usiku ya Jumamosi kuzunguka mji wa Johannesburg pekee. Akiwa chini ya mbinyo kuzuwia kurudiwa mauaji yaliyotokea mwaka 2008, Zuma alisafiri kwenda Durban kutembelea kambi wanayohifadhiwa wageni waliokimbia makazi yao kutokana na ghasia hizo, lakini alikabiliana na mapokezi yasiyokuwa mazuri kutoka kwa kundi lililomsubiri, ambalo lilipaaza sauti, "rudi nyumbani, rudi nyumbani" na umechelewa, umechelewa".
"Kama serikali , hatuwaambii nendeni zenu". Sio kila raia wa Afrika kusini anasema, nendeni zenu". Ni idadi ndogo sana ya watu ambao wanasema hivyo," Zuma amesema katika kambi ya Chatsworth, ambako alikabidhi hundi ya dola 4,100 kuwasaidia wahanga wa ghasia za chuki dhidi ya wageni.
Ameahidi kumaliza ghasia hizo na alilihakikishia kundi hilo la watu kwamba kuna nafasi kwa wageni nchini Afrika kusini. "Hata kama kuna wale wanaotaka kurejea nyumbani, wafahamu kwamba wakati tutakapositisha ghasia wanakaribishwa kurejea, " Zuma amesema.
Zuma afuta ziara
Kiongozi huyo wa Afrika kusini alitarajiwa kusafiri kwenda Indonesia jana Jumamosi, lakini alitangaza kufuta ziara hiyo "kushughulikia suala hilo nyumbani linalohusiana na mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni."
Uamuzi huo umekuja wakati hali ya tahadhari inaongezeka nchini Afrika kusini---na kutoka Umoja wa Mataifa pamoja na miji mingine mikubwa-- kuhusiana na mashambulio hayo.
Nchi jirani za Zimbabwe , Malawi na Msumbiji zimetangaza mipango ya kuwaondoa raia wake. Ikiakisi wasi wasi wa kimataifa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR limesema wahanga wengi walioshambuliwa, "ni wakimbizi na wanaohitaji hifadhi ya kisiasa ambao wamelazimika kukimbia nchi zao kutokana na vita pamoja na kukamatwa."
Kinachoelekezewa kidole cha lawama kwa kiasi kikubwa kutokana na ghasia hizo ni hotuba mwezi uliopita iliyotolewa na mfalme Goodwill Zwelithini, kiongozi wa kabila la Wazulu, ambapo amewalaumu wageni kutokana na kiwango cha juu cha uhalifu nchini Afrika kusini na kusema ni lazima"wafunge virago na kuondoka".
Mfalme huyo amekuwa akisema maneno yake yametafsiriwa vibaya.
Wakati mzozo huo ukiendelea, Zuma ameyataka makanisa yote kufanya sala maalum kwa ajili ya amani na urafiki leo Jumapili.
"Tunafahamu kwamba wengi wa watu wetu wanaamini kuhusu haki za binadamu na amani na kwamba wanaheshimu utu wa kila mtu anayeishi katika nchi hii," amesema katika taarifa iliyotolewa jana Jumamosi.
"Wanafahamu kwamba mahali palipo na hali ya wasi wasi na tofauti, haya yanaweza kutatuliwa kwa njia ya Afrika kusini, kupitia majadiliano, na sio kupitia ghasia na ukandamizaji."
Hasira miongoni mwa mataifa jirani na Afrika kusini
Ghasia hizo zimezusha hasira katika mataifa mengine ya Afrika.
Nchini Msumbiji kundi la watu wapatao 200 siku ya Ijumaa lilizuwia kivuko cha kusini kati ya nchi hizo cha Lebombo, wakirusha mawe dhidi ya magari ya Afrika kusini.
Nchini Zambia , redio inayomilikiwa na mtu binafsi ilisitisha kupiga muziki wa Afrika kusini katika hatua ya kupinga mashambulizi hayo dhidi ya wageni. Na katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare, waandamanaji walifika katika ubalozi wa Afrika kusini kulaani kile walichokiita "mauaji ya kiwendawazimu na ya kikatili" dhidi ya Waafrika wenzao.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe pia amelaani ghasia hizo siku ya Jumamosi, akielezea "hali ya kushitushwa na kuchukizwa".
Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe
Mhariri: Sudi Mnette

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni