Jumatano, 2 Julai 2014

MAFUNZO JUU YA USIMAMIZI SHIRIKISHA WA MALIASILI YAFANYIKA IRINGA

 
MAFUNZO_6_8ea72.jpg
Msimamizi Mkuu wa mafunzo, Dr. Naima Besta kutoka shirika la Lawyers' Environmental Action Team (LEAT) akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa mafunzo ya ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii katika ushiriki wa wananchi katika usimamizi wa maliasili, ambapo moja ya malengo makuu ya mafunzo hayo ni kuijengea uwezo jamii kufahamu mwelekeo sahihi wa uwajibikaji jamii. (FRIDAY SIMBAYA)
MAFUNZO_3c5f2.jpg
Mkufunzi Hana Lupembe (kulia) akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii katika ushiriki wa wananchi katika usimamizi wa maliasili (misitu na wanyamapori) yanayoendelea VETA, mjini Iringa.
MAFUNZO_2_8e183.jpg
MAFUNZO_3_6b53d.jpg
Mkufunzi mwingine Franklin Masika akimsikiliza kwa makini mmoja ya washiriki wa mafunzo, Jovita Mzena wakati wa mafunzo ya kufundisha wakufunzi (trainers of trainers).
MAFUNZO_4_119b3.jpg
Mkufunzi Franklin Masika (kulia) na msimamizi mkuu wa mafunzo Dr. Naima Besta (katikati)wakimsilikiza mshiriki kwa makini wakati akichangia mada.
Mafunzo yanahusu ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii katika ushiriki wananchi katika usimamizi wa maliasili (misitu na wanyamapori).
Malengo makuu ya mafunzo
I. Ni kuijengea uwezo jamii kufahamu mwelekeo sahihi wa uwajibikaji jamii.
II. Kuelewa dhana ya mfumo wa uwajibikaji jamii katika usimamizi wa misitu na wanyamapori.
III. Pia kuelewa hatua tano za mchakato wa mfumo wa uwajibikaji jamii ikwa ni pamoja na mpango wa mgawanyo wa rasilimali, usimamizi wa matumizi, usimamizi wa uadilifu na usimamizi wa uangalizi.
Vilevile mafunzo ya ufuatiliaji na usimamizi wa uwajibikaji wa jamii yanalenga kuongeza uelewa juu ya zana za uwajibikaji na usimamizi wa jamii kwa kufuatilia kila hatua ya mchakato.
Hivyo basi ufualiaji wa uwajibikaji jamii unawezesha watoa huduma kwa jamii kutoa ufafanuzi, uthibitisho na uhalalisho juu ya mgawanyo wa raslimali za umma, utekelezaji wake na ufanisi/utendaji wake ili kuweza kufikia haki za msingi za binadamu/mwananchi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni