Silaha kubwa za Kivita AK 47
SILAHA za kivita zikiwamo za AK 47, SMG na nyingine zimekuwa zikiingizwa nchini kinyemela kutoka Kenya, imeelezwa.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Tarime/Rorya, Justus Kamugisha amethibitisha kuwa silaha hizo zimekuwa zikiingia nchini.
"Ndugu yangu mwandishi suala la hapa mpakani lina changamoto zake... kuhusu silaha kuingia Tanzania kutoka Kenya hilo lipo".
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Tarime/Rorya, Justus Kamugisha amesema silaha hizo zimekuwa zikiingia nchini kinyemela kupitia vichochoro na njia za panya ambazo ni vigumu kudhibiti kutokana na mazingira yake kuwa magumu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni