Jumatano, 22 Aprili 2015

MCHEZAJI WA AFRICA KUSINI AFARIKI DUNIA TFF YATUMA RAMBIRAMBI

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Afrika Kusini (SAFA) Dr. Danny Jordan kufuatia kifo cha nguli aliyewahi kuichezea timu ya Taifa ya nchi hiyo (BafanaBafana) John Lesiba "Shoe" Mashoeu kilichotokea jana Aprili 21.
Katika salamu zake kwa Dr. Jordan, Malinzi amesema nchi ya Afrika Kusini imepatwa na pigo kubwa katika tasnia ya mpira wa miguu, kufuatia kifo cha Mashoeu aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa Saratani ya Utumbo, na kusema watanzania wako nao pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo.

John Lesiba "Shoe" Mashoeu aliyezaliwa Disemba 18, 1965 nchini Afrika Kusini, alikuwa ni miongoni wa wachezaji wa nchi hiyo waliotwaa Ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 1996 nchini Afrika Kusini na baadae kushiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Ufaransa mwaka 1998.
Wakati wa uhai wake Mashoe alipata kuvichezea vilabu vya Giant Blackpool, Kaizer Chiefs, Amazulu na Alexandria United vya Afrika Kusini, na timu Gencleribirligi, Kocaeilispor, Fenerbahce na Busrsapor za Uturuki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni