Jumatano, 2 Agosti 2017

Mwizi apatikana amelewa ndani ya nyumba aliovunja

Mtu mmoja ameshtakiwa na maafisa wa polisi nchini Australia baada ya kuvunja na kuingia katika nyumba moja kabla ya kunywa shampeni na kulala kitandani.

 Mtu mmoja ameshtakiwa nchini Australia baada ya kuvunja na kuingia katika nyumba moja kabla ya kunywa shampeni na kulala kitandani.

Polisi wanasema jamaa huyo wa miaka 36 alivunja na kuingia nyumbani humo mjini Esperence, magharibi mwa Australia siku ya Ijumaa wiki hii.
Alilewa baada ya kunywa kinywaji hicho, kulingana na maafisa.
Mwenye nyumba hiyo alirudi nyumbani na kumkuta mwizi huyo akiwa amelala katika kitandani mwake.
''Alitoka nje na kuwapigia simu polisi ambao waliwasili na kumkamata mshtakiwa'', alisema sajenti Richard Moore kutoka kituo cha polisi cha Esperence.
Mtu huyo alipelekwa hospitalini baada ya kupatikana amelewa chakari alisema sajenti Moore.
Ameshtakiwa kwa wizi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni