Alhamisi, 3 Agosti 2017

KWA WANAOTAKA KUOA: Bibi harusi ajaribu kumuua mumewe baada ya ndoa


 Bibi harusi wa mji wa Tennesse nchini Marekani aliyejaribu kumuu mumewe

 Bibi harusi wa mji wa Tennesse nchini Marekani aliyejaribu kumuu mumewe
Bibi harusi katika jimbo la Tennessee nchini Marekani ametiwa nguvuni baada ya polisi kusema kuwa alitoa bunduki kwenye gauni lake la harusi na kumtishia mumewe saa chache tu baada ya kufunga ndoa.
Kate Elizabeth Prichard, mwenye umri wa miaka 25, alikuwa bado amevalia gauni la harusi wakati alipokamatwa katika hoteli moja katika mji wa Murfreesboro.
Alidaiwa kuchukua bastola, na kuiweka kwenye kichwa cha mumewe na kufyatua.
Bahati nzuri bastola hiyo haikuwa na risasi, lakini baadaye alidaiwa kuijaza risasi na kufyatua angani, jambo lililowafanya waliokuwa wakishuhudia tukio hilo kukimbia.
Walioshuhudia tukio hilo waliandikisha taarifa kwa polisi ndipo polisi walipowasili eneo la tukio.
Walisema wawili hao walikuwa wakinywa pombe nje ya hoteli.
Sajenti polisi katika mji wa Murfreesboro Kyle Evans alisema kuwa maharusi hao wote wawili hawakushirikiana na mamlaka.
"Alivuta bastola kutoka kwenye gauni lake la harusi," Sajenti Evans aliviambia vyombo vya habari vya eneo hilo "akaielekeza kwenye kichwa cha mume wake na kufyatua"
Maafisa walimfahamisha mumewe kwamba fungate imeisha na mkewe mpya anakwenda jela " aliongeza Sajenti Evans
Sajenti Evans alisema kuwa bibi harusi alijaribu kuficha silaha bafuni katika hoteli walimokuwa lakini ikakamatwa.
Maoni yangu wanandoa wapimwe akili zao kabla ya ndoa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni