Polisi nchini
Afrika Kusini wametibua jaribio la kusafirisha gari moja la kifahari
lililokuwa limeibwa kwenda nchini Zimbabwe kwa kutumia punda kupitia mto
Limpopo.
Washukiwa walitoroka kwenda vichakani kueleka upande wa Zimbabwe baada ya jitihada za kulikwamua gari hilo lililokwama kwenye
mchanga kushindikana.Disemba iliyopita gari lililokuwa limeibwa kutoka mjini Durban lilipatikana katika mto huo huo likiwa limefungiwa kwa kutumia kamba kwa kundi la punda.
Polisi wanachunguza ikiwa kuna genge linalohusika na wizi huo.
Mto Limpopo ndio mpaka kati ya Afrika Kusini na Zimbabwe na ni maarufu kama njia wanayopitia wahamiaji haramu kati ya nchi hizo mbili, lakini kingo za mto huo kupitisha magari yaliyoibwa ni za kushangaza kutokana na mchanga mwingi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni