KISA CHA MWAKA MPYA 2014: SAMAKI AINA YA SATO AONYESHA MAAJABU WILAYA YA BUNDA, AINGIA TUMBONI MWA MSICHANA WA MIAKA 12 KUPITIA SEHEMU ZA SIRI
MAISHA ya mwanafunzi
wa kike mwenye umri wa miaka 12, (jina tunalihifadhi), anayesoma darasa la tano
Shule ya Msingi Bwanza, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, yako hatarini baada ya
kurukiwa na samaki aina ya sato, kuingia sehemu ya siri na kukimbilia tumboni.
Tukio hilo limetokea
Januari mosi mwaka huu, saa 11 alfajiri,wakati mtoto huyo akichota maji katika
Ziwa Victoria ili aweze kumwagilia bustani ya nyanya, vitunguu iliyopo
kandokando ya ziwa hilo.
Akizungumza na
Majira, kaka wa mtoto huyo (jina tunalihifadhi), mwenye miaka 31, alisema tukio
hilo limewashangaza wakazi wa Kijiji cha Bwanza na vitongoji
vyake.
Alisema mdogo wake
alikuwa akichota maji katika ziwa hilo akiwa amechuchumaa ndipo samaki huyo
anayedaiwa kuwa mwenye ukubwa wa nchi nne, aliruka kutoka majini, kuingia sehemu
yake ya siri na kukimbilia tumboni.
"Mdogo wangu alifanya
jitihada za kumvuta ili aweze kumtoa lakini alikimbilia tumboni na kuanza kupata
maumivu makali, kutokwa na damu nyingi baada ya kuparazwa na miiba ya mgongo
wa samaki huyo.
"Baada ya tukio hilo,
alirudi nyumbani kwa shida akijivuta na kuugulia maumivu...alimweleza mama na
ndugu zake juu ya mkasa huu, walimchunguza na kujaribu kuingiza mkono sehemu za
siri wakidhani watampata lakini hawakufanikiwa," alisema.
Aliongeza kuwa, baada
ya kumpeleka zahanati iliyopo kijijini hapo, hali yake ilizidi kuwa mbaya
akilalamika maumivu makali tumboni ambapo familia inaamini tukio hili limetokana
na imani za kishirikina hivyo waliamua kumtoa katika zahanati
hiyo.
"Tulimpeleka kwa
mganga wa kienyeji kijiji cha Amuyebe, wilayani Ukerewe...katika hali ya kawaida
samaki hawezi kumrukia mtu sehemu yake ya siri na kuzama
tumboni.
"Pamoja na kuchukua
uamuzi wa kumpeleka kwa mtaalamu, hali yake bado inazidi kuwa mbaya, hata baba
yetu alifariki katika mazingira yenye utata mwaka 2003,"
alisema.
Aliongeza kuwa, hata
kaka zake watatu na mtoto huyo nao walifariki kwa mfululizo mwaka 2004, 2005,
2006 ambao vifo vyao viligubikwa na utata mkubwa.
Mwenyekiti wa
Kitongoji cha Alwego anakoishi mtoto huyo, Bi. Reticia Bituro, alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambalo limewashangaza watu na kuahidi uongozi wa
kitongoji hicho utaendelea kufanya uchunguzi zaidi.
Diwani wa Kata ya
Napindi, Bw. Elias Magoti ambaye yuko safari kuhudhuria kikao cha Baraza la
Madiwani Bunda Mjini, alikiri kupokea taarifa za tukio hilo kwa mshangao
mkubwa.
"Nitalifuatilia kwa
karibu baada ya kurudi kijijini kwa kufanya uchunguzi ili kubaini kilichotokea
kwani sijawahi kusikia tukio kama hili katika umri nilionao,"
alisema.
Taarifa
zilizopatikana kutoka Ukerewe anakotibiwa mtoto huyo, zilisema kwa sasa hawezi
kuzungumza akizidi kulalamika maumivu makali ya tumbo na samaki huyo bado
hajatolewa. MAJIRA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni