Ijumaa, 16 Mei 2014

JK AHANI MSIBA WA MTOTO WA SALVA RWEYEMAMU

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipa pole Bibi Isabela Salva Rweyemamu ambaye ni mama wa Marehemu Private Brian Salva Rweyemamu wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa marehemu Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akiwafariji Mkurugenzi wa Mawasiliano Ofisi ya Rais Ikulu Bwana Salva Rweyemamu na Mkewe Isabela Salva Rweyemamu ambao ni wazazi wa Marehemu Private Brian Salva Rweyemamu nyumbani kwao Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kuifariji familia ya Marehemu Private Brian Salva Rweyemamu nyumbani kwao Kinondoni jijini Dar es Salaam leo (picha na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ofisi ya Rais Ikulu Bwana Salva Rweyemamu Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye Private Brian Salva Rweyemamu kilichotokea jana katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini baada ya kuugua kwa muda mfupi. Marehemu Private Brian anatarajiwa kuzikwa kesho mchana (Jumamosi) katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni