Kuna dalili ya uhai
kutoka katika mgodi wa dhahabu kufuatia ajali wiki iliyopita, ambapo
watu watatu walifunikwa, waokoaji anasema.
Wachimbaji mgodi watatu
wamekwama katika chumba cha taa, baada ya mgodi huo kuporomoka kufuatia
kisa ambapo jumba moja lililoko karibu na mgodi huo lilipoporomokea
mgodi huo siku ya ijumaa.Kundi la waokoaji linasema kuwa walisikia mlio wa ukuta ambayo huwa ni ishara ya mawasiliano kati ya wachimba mgodi wakiwa hatarini.
Ishara hiyo ya mawasiliano imeinua matumaini ya wenye mgodi huo kuwa wachimbaji mgodi walioko ardhini wangali hai.
Wafanyakazi zaidi ya 70 wa mgodi huo walifanikiwa kutoka kutoka chini ya ardhi kwa kutumia njia maalum ya dharura baada ya ajali hiyo kutokea Ijumaa katika Lily Mine karibu na mji wa kaskazini mashariki wa Barberton .
Ajali hiyo ilisababishwa na jumba lililoporomokea mgodi huo na kusababisha tani kadhaa za kifusi kuharibu mgodi huo na kufunikia wafanyikazi ardhini
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni