Simu za kisasa zinazotumia mfumo wa Android zinaweza kufuatiliwa kwa urahisi sana.
Uchnguzi umebaini kuwa simu zinazotumia mfumo huo zinaweza kufuatiliwa kwa urahisi mno pasi na kutumia kifaa cha GPS yake.Aidha simu hizo zinaweza kudukuliwa kwa kutumia matumizi ya betri yake huku utafiti ukisema kuwa simu zinazotumika karibu na kifaa cha kupeperushia masafa ya simu za kuungia mbali.
Simu za kisasa ''Smartphone'' hutumia nguvu zaidi inapokuwa mbali zaidi na kifaa hicho cha kupeperushia masafa ya GSM, kwani ina changamoto tele za kung'amua masafa.
Matumizi ya nguvu zaidi ya shughuli zingine yanaweza kubainishwa na ''alogarithm'' muundo msingi wa simu yenyewe.
Watafiti hao sasa wameunda mfumo ambao unakusanya habari kuhusu matumizi ya betri ya simu.
‘’Mfumo huo hairuhusu kutumia GPS wala huduma zozote kwa mfano mtandao wa Wi-fi ‘’
Jopo hilo linajumuisha Yan Michalevsky, Dan Boneh na Aaron Schulman kutoka idara ya sayansi ya tarakilishi katika chuo kikuu cha Standford pamoja na Gabi Nakibly kutoka kwa kampuni ya Rafael walioandika matokeo ya utafiti wao.
‘’Tuna ruhusa ya kuunganisha mtandao na upatikanaji wa nguvu yake.’’
‘’Hizi ni ruhusa za kawaida kwa mfumo huo na inawezekano wa kutoleta huduma kwa upande wa mwathiriwa.
Kuna mifumo 179 ambazo zinapatikana kwenye Anaroid, timu hiyo iliongezea.
Shughuli kama kusikiza muziki au kutumia mtandao wa kijamii inamaliza betri ya simu lakini hii inaweza kupunguzwa kutokana na ‘’kujifunza kwa mashine’’ripoti inasema.
Jaribio hilo lilifanyiwa kwa simu ambazo zinatumia mtandao wa 3G lakini haikuweza kupima nguvu kwa kuwa takwimu zinalindwa na kifaa hicho. BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni