Malala na mmoja wa wazazi wa wasichana waliotekwa nyara
Nigeria
Mwanaharakati mwenye umri mdogo raia wa pakistan Malala
Yousafzai amekutana na rais wa Nigeria Goodlack Jonathan mjini Abuja.
Lengo la mkutano huo ilikuwa kwa Malala kushinikiza Rais Goodluck kuchukua
hatua zaidi ili kuwakoa wasichana wa shule waliotekwa na kundi la wanmgambo wa
Boko Haram mwezi April.
Tayari mwanaharakati huyo ashakutana na familia za wasichana hao kuwapa moyo
na matumaini.
Boko Haram wametoa kanda ya video ya kusuta kampeni za kutaka kuachiliwa
wasichana hao. Kundi limetaka kuachiliwa kwa wapiganaji wake.
Malala alipigwa risasi kichwani na kundi la Taliban nchini Afghanistan
alipokuwa akipigania elimu kwa wasichana.
Malala mwenyewea alikuwa mwathiriwa wa vita vya Taleban nchini Pakistna ambao
na wao pia wanapinga elimu kwa watoto wasichana.
Yuko nchini Nigeria kwa ziara ya siku tatu. Katika siku ya kusherehekea siku
yake ya kuzaliwa, ameamua kwenda Nigeria kutoa wito wa kuwachiliwa kwa wasichana
hao wengi ambao wana umri sawa na yeye, miaka 17.
Ni miezi mitatu tangu wasichana hao zaidi ya 200 kutekwa nyara na pia sio
kawaida kwamba Rais Jonathan bado hata hajakutana na familia za wasichana hao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni