Jumanne, 9 Septemba 2014

MARIN CILIC BINGWA MPYA WA US OPEN

Marin Cilic wa Croatia ameibuka bingwa wa US Open kwa kumfunga Kei Nishikori wa Japan

Mpambano huo umechezwa katika uwanja wa Arthur Ashe Mjini New York Marekani.

Cilic amepokea kombe la michuano ya tennis upande wa wanaume kwa mara ya kwanza baada ya kumshindilia mpinzani wake seti tatu za 6-3, 6-3 , 6-3.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya fainali za US Open ambapo mchezo wa mwisho unawakosa mmoja kati ya wachezaji wakali akiwemo Andy Murray, Novak Djokovic ama Roger Federer.

Cilic anakuwa Mkroatia wa kwanza kutwaa ubingwa wa moja kati ya mashindano makubwa manne ya tenis duniani tangu kocha wake Goran Ivanisevic abebe ubingwa wa Wimbledon mwaka 2001.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni