Mgeni
Rasmi Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya
Kamani (wa tatu kushoto) pamoja na wageni wengine waliohudhuria Sherehe
hizo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uchumi, Jeshi la Kujenga
Taifa Kanali Felix Samilani, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja
Jenerali Raphael M. Muhuga, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe. John
Henjewele, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara, na Mkuu wa Kiteule cha Bulamba
Meja David Msakulo.
Mgeni
Rasmi Waziri wa Maendeleao ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya
Kamani (MB) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa Ufugaji wa
Samaki ndani ya Ziwa Viktoria Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia
mpya ya vizimba (Cages). Kushoto
ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe.John Henjewele, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Mara. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali
Raphael M. Muhuga.Waziri
wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani
akipandikiza vifaranga vya samaki ndani ya Ziwa Victoria, mradi
unaotekelezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya Bunda, Kiteule
cha Bulamba kwa kutumia teknolojia mpya hapa nchini ya kuzalisha samaki
kwenye vizimba.
Picha
ya vizimba ambavyo ufugaji wa samaki umeanza mara baada ya Waziri wa
Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kuzindua mradi huo na kupandikiza vifaranga
vya samaki. Mradi unatekeleza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya
Bunda, Kiteule cha Bulamba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
wakiwemo Economic Social Research Foundation (ESRF),
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Ofisi ya Rais, Tume
ya Mipango. Ufugaji wa samaki kwa kutumia teknolojia ya vizimba ndani ya
Ziwa Victoria, umekuwa ukitekelezwa pia na wenzetu wa Kenya na Uganda
ambao wamepiga hatua kubwa .
Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Mratibu Mwandamizi
wa Mradi Bw. Nehemia Murusuri (wa kwanza kulia) pamoja na Mwakilishi wa
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Mratibu wa Mradi wa Kuondoa Umaskini,
Kukuza Uchumi na Utunzaji Endelevu wa Mazingira, Bw. Telesphory
Kamugisha (wa pili kulia). Wengine ni baadhi ya wageni waliohudhuria
sherehe hizo.Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael M. Muhuga
akiongea na wananchi wa Kijiji cha Bulamba wakati wa Uzinduzi wa Mradi
wa Ufugaji wa samaki katika Ziwa Victoria kwa kutumia teknolojia ya
vizimba (Cages) ambayo ni teknolojia mpya ndani ya nchi yetu.Waziri
wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani akitoa
hotuba kwa wananchi wa kijiji cha Bulamba (hawapo pichani) mara baada ya
kuzindua Mradi wa Ufugaji wa Samaki ndani ya Ziwa Viktoria.
Aliwasisitiza wananchi kujiunga katika vikundi ili kujijengea uwezo wa
kuanza kutumia teknolojia ya kisasa ya kuzalisha samaki kwa kutumia
vizimba (Cages) katika ziwa Victoria.Waziri
wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (mwenye
Kaundasuti nyeusi) akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma ya asili
mara baada ya uzinduzi wa mradi huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni