BALOZI WA MAREKANI KWA KUCHOMWA KISU
Balozi Mark Lippet akiwa na majeraha baada ya shambulizi.
Balozi wa
Marekani nchini Korea Kusini ameshambuliwa kwa kisu usoni na pia katika
kifundo cha mkono wake na mshambuliaji aliyekuwa akibwata kuhusiana na
suala la kugawanywa kwa kipande cha ardhi ya serikali yao.
Mara tu
baada ya shambulio hilo Rais wa Marekani Barack Obama amemtakia uponaji
wa haraka msaidizi wake huyo wa zamani Mark Lippert akimuombea uponaji wa
haraka baada tu ya shambulio lililofanywa wakati wa hotuba ya asubuhi.
Balozi
huyo mwenye umri wa miaka 42 alikimbizwa hospitalini ambako alifanyiwa
upasuaji wa zaidi ya saa mbili ingawa madaktari wamethibitisha majeraha
yake hayatarishi maisha yake.
Jeraha
lake limekadiriwa kuwa na sentimeta kumi na moja upande wa kushoto na
ameshonwa nyuzi themanini kwenye mkono uliokatwa katika shambulio
lililosababisha baadhi ya mishipa kushindwa kufanya kazi. Msemaji wa
Ikulu ya Marekani amelaani kitendo hicho kwa nguvu zote.
Baada ya
shambulio hilo maofisa wa polisi walionekana wakimrukia na kumdhibiti
mshambuliaji aliyekuwa na kisu chenye urefu wa inchi kumi.
Polisi
wamemtambua mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 55 aitwaye Kim
Ki-Jong, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya shambulio kama hilo kwa
kumshambulia balozi wa Japan mjini Seoul mnamo mwaka 2010.
Mkuu wa
polisi Yoon Myung na amesema kwamba wanamshikilia mtuhumiwa huyo na
wanachunguza sababu ya shambulio hilo na masuala mengine kumhusu .Askari wakiwa wamemzunguka Balozi aliyejeruhiwa
Naye
msemaji wa baraza la maridhiano na ushirikiano ambaye alikuwa ndiye
muandaaji wa mkutano huo, ameomba radhi kwa kutokuwa na ulinzi madhubuti
.
Balozi
Lippert, ni mshauri wa muda mrefu wa Raisi Obama na ambaye pia aliwahi
kuwa msaidizi wa katibu mkuu wa ulinzi katika masuala ya mahusiano na
bara la Asia, na alipata nafasi ya kuwa balozi Korea Kusini mwezi October
mwaka wa jana.
Lippert
amewahi pia kushika wadhifa wa afisa wa usalama wa taifa katika
operesheni maalum na alitwaa medali ya nyota ya shaba nyeusi wakati
alipoitembelea Iraq.
Korea
Kusini na Kaskazini walitengana tangu mwaka 1950-53 baada ya vita vya
Korea na bado kiufundi wako vitani kwa kuwa mapigano yalisitishwa kwa
suluhu .
Marekani
na Korea Kusini wameunganisha nguvu za kijeshi na wiki hii wako katika
mazoezi kufuatia hali tata ya kiusalama kutoka kwa wakomunisti walioko
Kaskazini .
Pyongyang
wanadai kuwa wanafanya mazoezi kwa kujiweka tayari na uvamizi wowote
utakaotokea. Wakati huo huo Korea Kusini na Marekani wanadai kuwa
mazoezi yao ni kwa kujihami tu .
Marekani inakadiriwa kuwa na vikosi vya askari wake wapatao 30,000 vya kudumu vilivyopiga katika kambi za Korea Kusini.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni