WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali itatumia shilingi bilioni 55
kuvipatia umeme vijiji 244 vya mkoa wa Mbeya kupitia Miradi ya Umeme
Vijijini (REA).
Ametoa
kauli hiyo jana (Jumatatu, Machi 2, 2015) wakati akizungumza na
viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mbeya waliofika kusikiliza majumuisho ya
ziara yake ya siku saba kwenye mkoa huo. Mkutano huo ulifanyika kwenye
ukumbi wa Mkapa, jijini Mbeya.
“Nimeambiwa
kuwa katika mwaka 2014/15, jumla ya vijiji 244 vitapatiwa umeme kupitia
REA. Vijiji hivyo ni kama ifuatavyo: Chunya viko 13, Mbeya ni 32,
Mbarali (56), Mbozi (14), Momba (15), Kyela (30), Ileje (18) na Rungwe
(66) na jumla ya shilingi bilioni 55/- zitatumika kwa madhumuni hayo,”
alisema.
Waziri
Mkuu alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi wa mkoa huo kwa kusimamia
suala la usambazaji wa umeme vijijini na kukamilisha awamu ya kwanza ya
miradi ya umeme vijijini katika vijiji 17 vya mkoa huo.
“Nimeelezwa
kuwa miradi hiyo iliyogharamu ya shilingi billioni 7.6 katika vijiji 17
imekamilika kwa asilimia 100. Katika Halmashauri ya Mbeya kuna vijiji
vitano, Mbozi vijiji vinne, Chunya vijiji sita na Rungwe vijiji viwili;
na imeweza kuunganisha wateja 650,” alisema.
Alisema
taarifa zinaonesha kuwa vijiji vilivyopangwa kupata umeme wa REA mwaka
2015/2016 ni 51 na kwamba hivi sasa ujenzi wa njia kubwa ya umeme wa
11Kv na 33Kv unaendelea. “Pia ujenzi wa njia ndogo ya umeme 400v
unaendelea kujengwa na utekelezaji wa miradi hiyo umefikia asilimia
42.3,” aliongeza.
Aliwahimiza viongozi wa mkoa huo kuongeza jitihada za kusambaza umeme kwa kuwa mahitaji ya umeme ni makubwa kwa wananchi wengi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni