Jumapili, 31 Mei 2015

WAKULIMA NJOMBE WANAOGOPA MIKOPO

Baadhi ya wananchi wamedaiwa kuogopa mikopo kutoka halmashauri ya mji wa Njombe wamesema kuwa pesa hizo ni dili na kuogopa kutumia fursa hiyo.
Forum cc yaendelea yaendesha semina ya siku mbili katika ukumbi wa chuo cha maendeleo ya wananchi FDC Njombe.
Akizungumza wakati wa matembezi ya mafunzo baada ya mafunzo ya ndani ya kilimo biashara na utunzaji wa mazingira ambacho kimetolewa na taasisi ya Forum CC kwa kushirikiana na taasisi ya Seco Njombe, afisa mtendaji wa kata ya Luponde, Stanley Mkondola alisema kuwa wananchi kwa sasa wamekuwa waoga kuchukua mikopo kutoka halmashauri.

Amesema kuwa wananchi walio na uelewa wanaotakiwa kuonesha mfano katika uoneshaji wa vitendo katika kilimo biashara ambapo watawashawishi na walio katamaa.
Nao wakulima kutoka katika kata mbalimbali wakiwakilishwa na Panusi Mgaya amesema kuwa walishawahi kuchukua mkopo na kuwa walipo ingia katika mikopo walikatishwa tamaa kama anavyo eleza.
Naye afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya mji Yohana Kalinga amesema kuwa serikali imeandaa mkopo kwa wakazi wa kata mbalimbali zitakazo onesha mwitikio wa kufanya maendeleo.
Seco ikiwakilishwa na mkurugezi wake Luka Mgaya amesema kuwa taasisi hiyo ita ungana na Forum CC kwa kuwawezesha wananchi watakao onesha uwezo baada ya kupata mafunzo hayo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni