Vizuizi vya polisi vikiwaka moto mjini Pretoria.
Polisi nchini Afrika Kusini wanajaribu kuzuia ghasia ambazo zimetokea maeneo ya mji mkuu wa nchi hiyo Pretoria.
Taarifa
ya serikali ambayo inataka kuwepo utulivu na inasema kuwa maafisa wa
polisi walifyatuwa risasi wakati waandamanaji waliposhambulia gari lao
kwa mawe.Ghasia zilianza katika eneo la Tshwane kutokana na suala la mgombea wa kiti cha meya ambaye aliteuliwa na chama cha ANC kugombea uchaguzi mwezi Agosti.
Vyombo vya habari nchini humo vinaonyesha vizuizi vinavyowaka moto.
Serikali ya Afrika Kusini imeomba kufanyika kwa mazungumzo ili kusuluhisha tatizo hilo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni